MEGMET PATIENT GUIDES
Jipange vizuri kabla ya safari ya matibabu.
Miongozo mifupi ya kukusaidia kuwasilisha case yako, kulinganisha gharama na kujiandaa kwa safari salama.
01PATIENT GUIDE · 5 MIN
Jinsi ya kuandaa medical reports
Hospitali inaweza kutoa jibu zuri zaidi ikiwa case imewasilishwa kwa mpangilio na documents muhimu.
- Andaa summary ya daktari yenye diagnosis, dalili, matibabu uliyopata na sababu ya referral.
- Ambatanisha vipimo vya hivi karibuni, imaging reports na CD au picha za scan inapohitajika.
- Taja dawa zote unazotumia, allergies, magonjwa mengine na upasuaji uliowahi kufanyiwa.
- Tumia PDF au picha zinazoonekana vizuri na andika jina pamoja na tarehe kwenye kila document.
02PATIENT GUIDE · 5 MIN
Kuelewa makadirio ya gharama
Estimate ya matibabu ni mwongozo wa awali; kiasi cha mwisho kinaweza kubadilika baada ya daktari kumchunguza mgonjwa.
- Uliza kama estimate inajumuisha daktari, theatre, implant, dawa, ICU na siku za kulazwa.
- Thibitisha gharama za vipimo vya ziada, blood products, complications na kuongeza siku hospitalini.
- Omba muda ambao estimate itakuwa valid na namna ya malipo inayokubalika.
- Tenganisha gharama za hospitali na za visa, tiketi, malazi, chakula na usafiri wa ndani.
03PATIENT GUIDE · 5 MIN
Checklist ya safari ya matibabu
Mpango mzuri hupunguza usumbufu na husaidia mgonjwa kuendelea na matibabu bila mapengo.
- Thibitisha appointment, passport, visa na mahali pa kukaa kabla ya kununua tiketi isiyobadilika.
- Beba dawa za kutosha kwenye original packaging pamoja na prescription au barua ya daktari.
- Panga escort ikiwa mgonjwa anahitaji msaada wa kutembea, mawasiliano au maamuzi ya afya.
- Kabla ya kurudi, omba discharge summary, prescriptions, follow-up plan na mawasiliano ya timu ya matibabu.